ARSENAL KUPATA HUDUMA YA DANNY WELBECK NI MPAKA JANUARI



ARSENAL KUPATA HUDUMA YA DANNY WELBECK NI MPAKA JANUARI

STRAIKA wa Arsenal, Danny Welbeck ana matumaini ya kurejea tena katika kikosi hicho kuanzia januari, baada ya kukosekana uwanjani kwa muda mrefu kutokana na majeraha yanayomkabili.

Staa huyo wa zamani wa Manchester United alifanyiwa upasuaji wa goti mapema Septemba, mwaka huu ili kumuondolea tatizo hilo ambalo limekuwa likimsumbua misimu kadhaa ya nyuma.

Akizungumza juzi, Welbeck alikiri kwamba anajisikia vibaya kuishuhudia Gunners akiwa nje ya uwanja, lakini akaeleza matumaini yake ya kurejea uwanjani baada ya Sikuku ya Krismasi.

"Ni vigumu kupanga siku maalum ya kurejea uwanjani, lakini nadhani itakuwa ni karibia na mwaka mpya," staa huyo aliliambia gazeti la Nation wakati alipohojiwa kuhusu tarehe ambayo anadhani atakuwa amerejea uwanjani.

"Baada ya kufanyiwa upasuaji wiki kaddhaa zilizopita, najisikia vizuri, jambo ambalo linanipa matumaini hayo," aliongeza nyota huyo.


Comments