ARSENAL ATETEA UAMUZI WA KUCHEZESHA CHIPUKIZI KWENYE MECHI YA KIPIGO CHA 3-0 KUTOKA KWA SHEFFIELD WEDNESDAY ...lakini akiri walikuwa si lolote uwanjanii
Arsene Wenger ametetea uamuzi wake wa kuwapumzisha wachezaji wazoefu wa Arsenal katika mchezo wa Capital One Jumanne usiku dhidi ya Sheffield Wednesday.
Katika mechi hiyo Arsenal ilichukua kipigo cha 3-0 na kutupwa nje ya michuano hiyo.
Wenger ameshutumiwa kwa kupanga wachezaji chipukizi wakiwemo Glen Kamara, Alex Iwobi na Ismael Bennacer.
Hata hivyo pamoja na Wenger kutetea uamuzi wake huo lakini amekiri kuwa chipukizi hao hawakuwa tayari kwa mechi ya kiwango hicho.
Kocha huyo alisema: "Hawakuwa tayari kwa michuano hii, hakuna hata mmoja kati yao, magoli mawili yalitokana na mipira iliyokufa. Hatukuwa na weledi.
"Tulimiliki mpira lakini tulikosa mipango thabiti. Tulipwaya eneo la kiungo"
Ismael Bennacer mwenye umri wa miaka 17 alishindwa kufurukuta
Glen Kamara (kushoto) akikabwa na Sam Hutchinson
Wenger alimpanga kwa mara ya kwanza Alex Iwobi dhidi ya Sheffield Wednesday
Wenger akifuatilia mchezo
Comments
Post a Comment