Huenda suala la muamuzi Mike Dean kuacha kuchezesha mechi za Arsenal likajadiliwa bungeni mara baada ya mashabiki kusaini petition ya kutokua na imani naye na kufikia saini laki moja.
Mike Dean aliwatoa kwa kadi nyekundu wachezaji Gabriel Paulista na Saint Carzola katika mchezo uliomalizika kwa Arsenal kulala mabao 2-0 mbele ya Chelsea weekend iliyopita huku akimuacha uwanjani mshambuliaji Diego Costa ambaye sasa FA wamemfungia.
Baada ya kutoridhishwa na maamuzi yake, mashabiki wa Arsenal walitengeneza petition ili isainiwe na wanaotaka Dean asichezehe tena mechi za Arsenal na sasa zimefikia laki moja.
Kwa utamaduni wa England, petition inayofikia saini laki moja hujadiliwa katika bunge la nchi hiyo. Lakini hiyo inawezekana tu kutegemeana na usiriazi wa jambo lenyewe na sio jokes 'utani'.
Comments
Post a Comment