WAYNE ROONEY AVUNJA REKODI YA MIAKA 45 YA BOBBY CHARLTON ENGLAND IKISHINDA 2-0 DHIDI YA SWITZERLAND


WAYNE ROONEY AVUNJA REKODI YA MIAKA 45 YA BOBBY CHARLTON ENGLAND IKISHINDA 2-0 DHIDI YA SWITZERLAND

Hatimaye Wayne Rooney amevunja rekodi ya Sir Bobby Charlton ya kuwa mfungaji mwenye magoli mengi zaidi katika timu ya taifa ya England baada ya kutupia mpira  wavuni kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Switzerland ndani ya dimba la Wembley.

Katika mchezo huo wa kufuzu Euro 2016 Rooney alifunga katika dakika ya 84 na kufisha magoli 50, moja zaidi ya magoli 49 ya Sir Bobby Charlton.

Rooney            said in his speech that he was keen to see younger players            like Tottenham's Harry Kane (left) experience a similar rise            to the top 
Nahodha huyo wa England alifikia rekodi ya Sir Bobby Charlton Jumamosi iliyopita pale alipofunga kwa mkwaju wa penalti kwenye karamu ya bao 6-0 dhidi ya San Marino.

Jumanne usiku Rooney kwa kupitia tena mkwaju wa penalti, akafunga dhidi ya Switzerland na kuweka rekodi mpya England baada ya miaka 45.
Wembley            Stadium erupts as the Manchester United striker's 50th goal            for England is confirmed on Tuesday night  

Bao lingine la England lilifungwa na Harry Kane dakika ya 67.

Kwa ushindi huo, England imejihakikishia nafasi ya kwanza ya kundi E baada ya kushinda mechi zake nane na kujikusanyia pointi 24 na sasa hata ikipoteza michezo yake miwili iliyosalia, bado itakuwa kileleni kwa kundi hilo.
Rooney is            presented a special shirt to mark his record goal tally by            England boss Roy Hodgson (left) in the home dressing room 


Comments