Watu 13 wamepoteza maisha yao baada ya mtumbwi walimokuwa wakisafiria kugongana na feri Idara ya kulinda fukwe za bahari ya Uturuki imetangaza.
13 wanadhaniwa kuwa ni wahamiaji.
Mtumbwi huo unaaminika kuwa ulikuwa ukielekea katika kisiwa cha Lesbos kilichoko ugiriki ajali hiyo ilipotokea.
Ajali yenyewe imetokea karibu na bandari ya Canakkale Uturuki.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Dogan mtumbwi huo ulikuwa na jumla ya watu 46.
20 kati yao waliokolewa majini huku wengine 13 wakiwa hawajapatikana.
4 kati ya wale waliokufa maji ni watoto.
Wakati huohuo idadi kubwa ya wahamiaji wanazidi kuelekea katika mataifa ya bara ulaya.
Foleni kubwa ya watu imeripotiwa kwenye mpaka kati ya Slovenia Austria na Croatia licha ya mikakati ya kuwazuia kuingia katika mataifa hayo.
Kuwepo kwao katika eneo hilo la Ulaya kumezua makabiliano baina ya Austria, Hungary na Croatia.
Comments
Post a Comment