WACHEZAJI WA CHELSEA WAINGIWA NA HOFU


WACHEZAJI WA CHELSEA WAINGIWA NA HOFU

momo

Wachezaji wa Chelsea wana wasiwasi kuhusu utetezi wa taji lao la EPL baada ya kuachwa points 11 nyuma ya wanaaongoza ligi kwa sasa ambao ni Manchester city. Jumamosi iliyopita Chelsea imeshuhudiwa ikichezea kichapo cha 3-1 kutoka kwa Everton.

Taarifa za tetesi kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo zinasema kwamba wachezaji wana hofu kuhusu gap ambalo lipo kati ya mabingwa hao na Manchester city ambao kwasasa wapo vizuri kwenye msimamo wa ligi.

Wakati huo huo Mourinho anaoneka kwamba haja panic na ameendelea ku-focus kwenye mechi ya Champions League nyumbani kwao dhidi ya MAccabi Tel Aviv.

Story hizo za wachezaji ku-panic zilipamba moto pale mchambuzi mmoja wa michezo Stan Collymore aliposema kwamba John Terry na Diego Costa waligombana wakiwa kwenye viwanja vya mazoezi lakini taarifa hizo zilikanushwa na uongozi wa Chelsea.



Comments