Magoli ya Theo Walcott na Oliver Giroud yalitosha kabisa kuwa Arsenal point 3 muhimu kwenye mechi dhidi ya Stoke city. Mchezo huo ulikua na baraka tosha baada ya manager Wenger kusema kwamba kila pound moja ya ticket ya mechi ile itaenda kwa wakimbizi wa Syria.
Alex Oxlade-Chamberlain na Calum Chambers walitumia mechi ya boxing kati ya Anthony Joshua Vs Gary Cornish ambae hakuwai kupigwa hapo zamani kama sehemu ku-enjoy baada ya mechi yao dhidi ya Stoke City. Boxing match hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa O2 arena na baadhi kati ya sura maarufu ni za wachezaji hawa wawili wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Calum Chambers.
Anthony Joshua alimpiga Gary Cornish ndani ya sekunde 97 tu na kushinda taji la Commonwealth.
Comments
Post a Comment