Vitu 4 vinavyoiangusha Liverpool chini ya Brendan Rogers



Vitu 4 vinavyoiangusha Liverpool chini ya Brendan Rogers

 Siku za utawala wa kocha Brendan Rogers ndani ya klabu ya Liverpool zimeanza kuhesabika baada ya mfululizo wa matokeo wanayopata Liverpool katika siku za hivi karibuni .

Liverpool mabingwa wa mara 18 wa ligi kuu ya England, waliendelea kuusotea ubingwa huo ambao mara ya mwisho kuuchukua miaka ni takribani 20 iliyopita, msimu uliopita walimaliza nje ya Top 4 na hivyo kukosa nafasi ya kushiriki katika michuano ya Champions League pamoja kufanya uwekezaji mkubwa katika usajili.

Msimu huu pia wameuanza vibaya pamoja na kuwekeza fedha nyingi kwenye usajili, wamecheza mechi 7, wakishinda 3, sare 2, na wakipoteza 2 – ukiwemo mchezo dhidi ya mahasimu wao Manchester United. Na baada ya mchezo watu wameanza kuishinikiza bodi kumtimua kazi. Lakini yote yametokana na mambo manne yafuatayo:

1) USAFIRI

  Moja ya matatizo makuu yanayoisumbua Liverpool ni usajili wa wachezaji wanaofanya. Rodgers amefanya usajili wa wachezaji wengi sana na wengi wao aidha amewatoa kwa mkopo au kawauza. Hajafanya usajili mzuri pamoja bajeti nzuri anayopewa. Mamilioni ya paundi yametumika kwa wachezaji ambao wameshindwa kuipa Liverpool ubora inaohuhitaji na ndio maana timu chini ya Rogers haijaweza kuendelea kwa mafanikio.
2) Matatizo katika Safu ya Ulinzi

  Liverpool wamekuwa na kiwango kibovu katika ulinzi katika miaka ya hivi karibuni. Safu ya ulinzi iliwagharimu ubingwa miaka miwili iliyopita- walikuwa na safu kali mno ya ushambuliaji lakini beki dhaifu. Waliruhusu magoli mengi mno. Usajili uliofuatia baada ya hapo hakusaidia pia. Dejan Lovren ameendelea ku-flop kila msimu na Sakho amekuwa usajili wa ghali ukilinganisha na mchango wake kwenye timu. Kimuundo Liverpool wapo wazi nyuma na wameruhusu magoli mengi msimu huu. Rogers amekuwa akibadili mfumo kwa kucheza na mabeki wanne au watatu na hilo halijaweza kuwa tiba. Muundo wa safu ya ulinzi haupo sawa.
3) Matatizo kwenye Ushambuliaji 

  
Luis Suarez alikuwa sababu kubwa ya kwanini Liverpool walifanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili miaka miwili iliyopita. Alifunika matatizo mengi katika timu hiyo na kwa hakika alikuwa 'world class talent', akiwa ndio mchezaji bora katika ligi. Kwa namna ya kipekee aliibeba Liverpool na kuisogeza kabisa katika ndoto ya kutwaa ubingwa. Alipoondoka, matatizo aliyokuwa akiyafunika yaliyoonekana wazi. Liverpool mpaka sasa hawajaweza kumsaini mchezaji mwenye uwezo wa kuwa mbadala wa Suarez, na sasa Christian Benteke ndio mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa fedha nyingi kuziba pengo la Suarez.

Majeruhi kwa Daniel Sturidge yamezidi kukuza tatizo, kwa sababu amekuwa muhimu katika kuisadia timu. Msimu kabla ya mechi wikiendi iliyopita walikuwa wamefunga magoli manne tu katika mechi 6.
4) Filosofi Isiyoeleweka

  
Rodgers anajiona kama kocha mwenye filosofia ya kiufundi inayoeleweka. Akiwa Swansea – timu ilikuwa ikicheza soka safi huku ikitawala mchezo  na walipata sifa kubwa kwa aina hiyo ya mchezo. Alipokuja Liverpool, walikuwa na kasi huku wakitawala mpira, mchezo uliopelekea kushindani ubingwa lakini tangu wakati huo hana filosofia ya ufundi inayoeleweka. Amekuwa akitumia mifumo mingi na akiwapanga wachezaji katika nafasi wasizozimudu, mfano Danny Ings akicheza kama winga au Markovic akicheza kama wing-back – mifumo hii imeharibu kuboreka kwa kikosi na kutokuonyesha kiuhalisia nini anataka kufanya. Kwa usajili wote aliofanya bado haipo wazi mchezaji gani anafiti kucheza sehemu gani na kwanini. Matatizo yote haya yanazalishwa na kutokuwa na sera nzuri ya usajili ambayo inamfanya asionekane kuwa na filosofia yenye kueleweka.



Comments