VAN PLUIJM, MKWASA, WAVAMIA AZAM COMPLEX KUZISOMA AZAM FC NA PRISONS Kocha mkuu wa Yanga Hans van der Pluijm (kushoto) akiwa na Charles Boniface Mkwasa (kulia) kocha msaidizi wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wakifatilia mchezo wa Azam dhidi ya Prisons
Wakati timu ya Azam FC ikimenyana na Tanzania Prisons kwenye dimba la Azam Complex, kocha mkuu wa Yanga SC Hans van der Pluijm pamoja na kocha msaidizi wa Yanga huku akiwa ni kocha mkuu wa Stars Boniface Mkwasa walikuwa ni miongoni mwa watu maarufu waliohudhuria uwanjani kufatilia mchezo huo.
Baada ya mchezo kumalizika, Van Pluijm alionekana akiteta jambo na kocha wa mkuu wa Azam FC Stewart Hall na baadae kuondoka kwenye uwanja huo.
Kocha mkuu wa Yanga SC Hans van Der Pluijm (kushoto) akiteta jambo na kocha mkuu wa Azam FC Stewart Hall mara baada ya mchezo kumalizika kati ya Azam FC dhidi ya Prisons
Wakati mchezo kati ya Azam dhidi ya Prisons unaendelea, kocha mkuu wa Yanga alikuwa makini kuusoma mchezo huo na alionekana wazi kunakitu cha kiufundi anakifatilia kupitia mchezo huo.
Van Pluijm akifatilia kwa makini mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Tanzaniz Prisons
Angalia picha nyingine za watu maarufu waliokuwepo kwenye mchezo huo jana jioni kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Salum Mayanga, Kocha wa timu ya Tanzania Prisons ya Mbeya
Kocha msaidizi wa Simba SC akiwa na makocha wengine wanaopata mafunzo ya ukocha pia alikuwepo kushuhudia mchezo wa kati ya Azam FC dhidi ya Tanzania Prison
Kocha mkuu wa Azam FC Stewart Hall akifurahia jambo na viongozi wa benchi la ufundi la Prisons baada ya mchezo wao kumalizika
Wachezaji wa Azam FC Shomari Kapombe na Frank Domayo wakifatilia kwa karibu mechi kati ya timu yao dhidi ya Prisons wakiwa jukwaani
Comments
Post a Comment