VAN GAAL AWAONYA MASHABIKI KUHUSU ANTHONY MARTIAL


VAN GAAL AWAONYA MASHABIKI KUHUSU ANTHONY MARTIAL

Football - Manchester United v Liverpool - Barclays              Premier League - Old Trafford - 12/9/15 Anthony Martial              celebrates after scoring the third goal for Manchester              United Action Images via Reuters / Carl Recine Livepic              EDITORIAL USE ONLY. No use with unauthorized audio, video,              data, fixture lists, club/league logos or "live"              services. Online in-match use limited to 45 images, no video              emulation. No use in betting, games or single              club/league/player publications. Please contact your account              representative for further details.

Kinda Anthony Martial jana alianza kuandika jina lake katika lipsi za midomo za mashabiki wa klabu yake mpya ya Manchester United mara baada ya kufunga goli katika mchezo wake wa kwanza, akitokea benchi dhidi ya Liverpool.

Katika mchezo huo mkubwa zaidi katika historia ya soka la England, Anthony Martial aliingia uwanjani katika dakika ya 65 kuchukua nafasi ya Juan Mata na wakati ubao unasomeka 2-1 Manchester United wakiwa mbele, Martial aliihakikishia ushindi timu yake baada ya kupachika goli zuri katika dakika ya 84 na kufanya matokeo kuwa ni 3-1.

Akitokea pembeni mithili ya Thierry Henry, kinda huyo aliwapiga chenga walinzi Martin Skirtel na Dejan Lovren kabla ya kufunga katika nyavu ndogo na kuibua hisia kubwa miongoni mwa mashabiki wa Manchester United.

Akiongea mara baada ya mchezo huo, kocha wa Man United, Louis Van Gaal amewataka mashabiki kutotarajia makubwa haraka toka kwa kinda huyo na badala yake amewataka wampe muda ili kumuondolea presha.

Van Gaal anasema, Martial amefunga goli zuri sana lakini ni vyema wakamchukulia kawaida kama ilivyokuwa kwa Cristiano Ronaldo ambaye alikulia klabuni hapo na baadae kuwa mchezaji bora wa dunia.

Wakati huo huo Van Gaal amesema anatarajia kumtumia nahodha wake Wayne Rooney katika mchezo ujao dhidi ya Southampton weekend na sio Jumanne hii katika UEFA dhidi ya PSV kwa maana anaogopa kumuongezea majeraha.

Maruane Fellaini alianza kama mshambuliaji wa kati na anatarajiwa kucheza tena hapo dhidi ya PSV Jumanne hii katika michuano ya klabu bingwa Ulaya, UEFA.



Comments