VAN GAAL AAHIDI KUICHAPA LIVERPOOL LAKINI AITAKA MANCHESTER UNITED ISAHAU UBINGWA MSIMU HUU ...ataka yan Giggs awe mrithi wake
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amewaambia mashabiki wake wasiwe na shaka juu ya mechi yao ya Premier League Jumamosi dhidi ya Liverpool kwa kusema" "Tutashinda Jumamosi".
Van Gaal ameyasema hayo ikiwa ni wiki chache baada ya kupokea kipigo cha 2-1 kutoka kwa Swansea.
Alipoulizwa kuhusu kichapo cha Swansea, Van Gaal akaseama: "Kumradhi, kipigo kile ni makosa yangu. Msijali tutashinda Jumamosi."
Hata hivyo Van Gaal ataacha maswali mengi kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kukiri kuwa hana matumaini ya kutwaa taji la Premier League msimu huu.
Van Gaal amedai matumani yake ni kumaliza katika nafasi ya tatu au ya pili, lakini ubingwa si msimuu huu labda kwa msimu ujao.
Kocha huyo wa Manchester United pia ameanza kumzungumzia mrithi wake kwa kusema anaamini Ryan Giggs ni mtu sahihi wa kuchukua nafasi yake pale atakapoondoka Old Trafford.
Louis van Gaal ameahidi ushindi dhidi ya Liverpool
Hata hivyo Van Gaal amesema hana matumaini ya kuwa mabingwa msimu huu
Comments
Post a Comment