Sasa hivi The Sun limetoka tena na story kuhusu Yaya Toure na mpenzi wake wa kimya kimya ambae amemzalisha hadi mtoto. Mwanamke huyo ambae amejitambulisha kwa jina la Mariam Camara amesema kwamba alikua na mapenzi na Yaya Toure kwa siri hadi pale aliposhika ujauzito na Yaya kumpotezea.
"Tulikua wapenzi na mambo yetu yalikua kwa siri ndani ya muda mrefu hadi pale nilipopata ujauzito. Nilipomwambia alikataa na nilivyojifungua alimkataa mtoto hadi tulipopima DNA akakubali. Baadae akaendelea kunitumia pesa za matumizi kwa ajili ya mtoto"
Sasa kitu cha ajabu ambacho mwanamke huyu anadai ni kwamba Yaya ana tabia kuleta masharti wakati wa kutuma pesa. "Yaya alikua ananipa masharti wakati wa kunitumia pesa hadi nimtumie picha za selfie nikiwa naonyesha jinsi gani nilivyo sexy. Nisipomtumia hizo selfie na pesa hatumi. Hivi sasa ameacha kabisa kunitumia pesa za matumizi kwasababu nimekataa hayo masharti ya kumtumia picha ndio anitumie pesa wakati ni jukumu lake bila hata kukumbushwa"
Mwanamke huyo anaendelea kumlea huyo mtoto wa kiume na Yaya Toure yupo Manchester na mke wake wanakoishi kama kawaida. Pia mwanamke huyo anasisitiza Yaya kawai kumuona mtoto wake mara mbili tu tangu azaliwe.
Comments
Post a Comment