UPO TAYARI KUMUANGALIA LEWANDOWSKI AKITUPIA GOLI LA 100


UPO TAYARI KUMUANGALIA LEWANDOWSKI AKITUPIA GOLI LA 100

sdszfbfsd

Kwenye mechi ya kesho ambayo ni Bayern Munich Vs Mainz mchezaji wa Bayern ana nafasi ya kuweka rekodi binafsi ya kufunga magoli 100 kwenye ligi ya Bundesliga.

Kwenye mechi iliyopita alifunga magoli 5 alifikisha magoli 99 na kwenye mechi inayofuata anahitaji goli 1 tu kufikisha magoli 100. Magoli yote haya 99 amefikisha akiwa anacheza kwenye club za Borussia Dortmund na Bayern. Akiwa na Borussia alitupia magoli 74 na akiwa na Bayern Munich ametupia magoli 25.

Watu wanasema Lewandowski ni mchezaji ambae ana chukuliwa poa sana lakini anatakiwa kupata heshima kama wanayopata wachezaji kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Mechi hii ambayo Lewandowski anaweza kutupia goli la 100 itaonekana live kupitia Startimes saa 10:30 jioni siku ya jumamosi September 26.



Comments