UNAJUA LUKE SHAW KAMWAMBIA NINI JAMAA ALIYEMVUNJA MGUU?



UNAJUA LUKE SHAW KAMWAMBIA NINI JAMAA ALIYEMVUNJA MGUU?

Luke Shaw 3Hector Moreno ameweka wazi kile ambacho ameambiwa na Luke Show alipokwenda Hospitali ambapo Shaw natibiwa siku ya Ijumaa iliyopita akiwa ameongozana na kocha wake Phillip Cocu.

Beki huyo wa kati wa PSV Eindhoven hakupewa adhabu yoyote licha ya kumuumiza Shaw kwa kumvunja mguu ambao atauuguza kwa miezi sita kabla ya kurejea uwanjani.

Moreno amesema: "kile kilichotokea kwa Shaw ilikuwa ni bahati mbaya. Na nilishtushwa sana".

Luke Shaw 4"Nimefurahi nimeweza kuzungumza nae, niliongoza na Philip Cocu kwenda hospilali kumtembelea. Kitu ambacho kilikuwa ni kigumu kwa mwanzoni, lakini alinipokea vizuri na hakunilaumu".

"Aliangalia picha na akasema ilikuwa ni sehemu ya mchezo. Kiauli hiyo ilinifanya nitabasamu".

Shaw alirejea Manchester siku ya Jumapili asubuhi akitokea Uholanzi ambako alikuwa anatibiwa mguu wake wa kulia uliovunjika mara mbili wakati timu yake ikipambana na PSV kwenye mchuano wa kombe la klabu bingwa Ulaya.

Luke Shaw 6Kwenye posti yake ya Jumamosi kwenye account ya Istagram mlinzi huyo wa aliwashukuru wafanyakazi wa hospitali ya St Anna Hospital mjini Eindhoven.

Aliposti picha tatu akiwa pamoja na wafanyakazi hao zilizoambatna na ujumbe uliosomeka: 'I just wanna say a massive thank you to everyone at St Anna hosptal for all the care and attention they have given me the last few days'. (Namshukuru kila mmoja kwenye hospitali ya St Anna kwa uangalizi walionipa siku chache zilizopita).

Luke Shaw 5



Comments