Ukiwatajia jina la Henry mashabiki wa Arsenal wanakumbuka moment nyingi nzuri ambazo aliwaletea kipindi chake anachezea club hiyo.
Sasa hivi Thierry Henry amepewa majukumu na ameisimamia club ya Arsenal ya vijana kwenye mazoezi wakati ikijiandaa na mashindano ya UEFA ya vijana dhidi ya Dinamo Zagreb.
Henry ambae anaongoza kwa kufunga magoli kwenye club ya Arsenal kuliko mchezaji yoyote, amefunga magoli 228 kwenye mechi 376 alizowai kucheza. Henry na kocha mwenzake wamesimamia mazoezi ya wachezaji wenye miaka under 19 wa club ya Arsenal ambao wanajiandaa na UEFA Youth League.
Wachambuzi wengi wanasema kwamba huu unaweza kuwa ni mwanzo wa safari ya Henry kuwa head coach wa Arsenal miaka ijayo.
Comments
Post a Comment