Carlos Tevez ameomba radhi baada ya kumvunja mguu kiungo wa Argentinos Juniors Ezequiel Ham wakati Boca Juniors ikishinda 3-1 Jumamosi usiku.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Juventus alifunga mara mbili katika mchezo huo lakini mchango wake huo ukafunikwa na tukio la simanzi pale alipomvunja Ezequiel Ham katika juhudi ya kupora mpira.
Tevez mwenye umri wa miaka 31 akasema baada ya mchezo huo: "Imeniuma sana kwa sababu nilikuwa nafuata mpira, sikukusudia kumuumiza, baada ya miguu yetu kukugusana nikajua nimefanya kitu cha hatari,"
Carlos Tevez akimpeleka mguu wake kwenye mguu wa Ezequiel Ham na kumsababishia ajali mbaya
Tevez ameomba radhi kwa tukio hilo
Comments
Post a Comment