Kiungo wa Argentinos Junior Ezequiel Ham amemshukuru nyota wa Boca Juniors Carlos Tevez baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa vilabu vya Ulaya kwenda kumtembelea hospital anakotibiwa Jumatatu usiku kufuatia tukio la kumvunja mguu uwanjani wakati timu zao zilipokuwa zikipambana.
Tevez alimvunja mguu Ham wakati wawili hao walipokuta wakaiwa wanawania mpira kwenye mchezo wa ligi kuu ya Argentina (Primera Dicision) ambapo Boca waliibuka na ushindi wa goli 3-0 huku picha za tukio hilo baya zikisambaa duniani kote.
Lakini inaonekana kama mchezaji huyo wa Argentinos amefurahishwa na Tevez kwenda kumjulia hali akiwa hospitali kwani aliposti picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa na nyota huyo wa Argentina Jumatatu usiku.
Picha hiyo iliandikwa: 'Asante Carlitos kwa kunitembelea'.Tevez aliomba radhi mapema baada ya kutambua maumivu ambayo amemsababishia Ham na akaamua kwenda kumtembelea hospitali.
"Inanifanya nijisikie vibaya kwasababu nienda kuchukua mpira, ilikuwa ni bahati mbaya sikukusudia kumuumiza. Baada ya kugusana nae kitendo kile kilinifanya nihisi nimefanya kitu kibaya", Tevez alisema baada ya kumalizika kwa mchezo.
Kocha wa Argentinos Nestor Gorosito alichelewa kukubali kwamba tukio hilo halikuwa la kukusudia kwa kuangalia namna Ham alivyoumizwa.
Haikuwa bahati mbaya, Gorosito aliiambia tovuti rasmi ya timu yak.Tulikuwa umbali wa mita tatu kutoka eneo la tukio na tuliwea kuona…kwa waliocheza mpira wanajua haya mambo".
Comments
Post a Comment