Mshambuliaji wa Yanga aliyetemwa Simba misimu miwili iliyopita Amis Tambwe amesema amefurahi sana kuifunga timu yake ya zamani na anajisikia amani kwa sasa kwasababu wapinzani wao waliongea maneno mengi kabla ya mchezo wao.
Tambwe ameongeza kuwa, wala hakuwa na 'mchecheto' na alicheza kawaida kama anavyocheza kwenye mechi nyingine lakini alikuwa na lengo la kuhakikisha anaisaidia timu yake ipate ushindi
"Nafurahi sana sana, tena sana kuifunga Simba, dakika 90 ndio zinaamua uwanjani, mwanasoka huwezi ukasema muda ufike tuwapige unatakiwa kujiandaa kwa kila mechi ili timu yako ishinde, alisema Tambwe.
"Mimi wala sikuwa na presha, nimeshacheza mechi kubwa nyingi kwahiyo kwangu mechi ya leo ilikuwa ya kawaida tu. Kwanza ukicheza kwa presha mpira utakushinda nilikuwa nacheza mpira wangu wa kawaida tu ule ambao huwa nacheza siku zote. Sikuwa nikicheza ili nionekane wala watu waniongelee".
"Simba walikuwa wanaongea sana kabla ya mchezo wa leo, walisema wametuandalia supu ya mawe na kachumbari ya miba na misumari, basi hiyo supu na kachumbari wakaile wao. Sisi tulibaki kimya tukajiandaa vizuri na leo tumeshinda ndio maana mimi nimefurahi sana".
Comments
Post a Comment