Mshambuliaji            Daniel Sturridge wa Liverpool ameweka rekodi ya kuwa na            wastani mzuri wa kufunga katika ligi kuu England ndani ya            klabu ya Liverpool baada ya kufunga mara mbili dhidi ya Aston            Villa weekend ya jana.
Sturridge ameifungia Liverpool magoli 37 katika mechi 57 alizoichezea klabu yake kati ya michezo ya ligi kuu ya England na kuweka wastani wa kufunga goli 0.65 kwa mechi na kuipita ile ya Fernando Torres wa 0.64.
Pamoja na majeruhi ya mara kwa mara, Sturridge amefunga magoli 42 kati ya michezo 69 aliyoichezea Liverpool katika mashindano mbalimbali.
Luis            Suarez aliifungia Liverpool magoli 69 kati ya michezo 110            akiwa na wastani wa kufunga goli 0.63
Michael Owen alifunga magoli 118 kati ya michezo 216 aliyoichezea klabu hiyo huku akiwa na wastani wa kufunga goli 0.55 kwa mechi.
Daniel Sturridge ana nafasi kubwa ya kuongeza wastani huo kwa kuwa bado ana muda mrefu zaidi wa kucheza klabuni hapo.
Comments
Post a Comment