STONES AWAONESHA CHELSEA, NINI WANAKIKOSA


STONES AWAONESHA CHELSEA, NINI WANAKIKOSA
John Stones

John Stones

Mlinzi kinda wa klabu ya Everton John Stones aliyekuwa akiwaniwa na Chelsea kwa muda mrefu hususan katika majira ya joto ameonesha uwezo wa hali ya juu timu yake ikiigaragaza Chelsea katika mchezo wa ligi kuu England.

Katika mchezo huo, Everton walishinda kwa jumla ya magoli 3-1 yote yakifungwa na mkongwe Naismith huku Nemanja Matic akifunga la kufutia machozi katika uwanja wa Goodson Park na kuwafanya Chelsea wasalie katika nafasi ya 15 na points zao 4 katika mechi 5 walizocheza.

Katika mchezo huo, Stones alipiga pasi complete 36 kati ya 41 alizopiga huku akifanya tacklings kwa asilimia 100. Lakini kwa upande wa pili wa Chelsea, John Terry hakupiga hata tackling moja katika dakika zote tisini.

Walinzi hao wa Chelsea, John Terry na Kurt Zouma walishindwa kabisa kuwazuia washambuliaji wa Everton hata kuruhusu mabao 3 langoni kwao na sasa wameruhusu magoli 11 katika mechi tano walizocheza.

Kwa upande wake Stones kama kawaida yake alicheza kwa nidhamu ya hali ya juu huku akifanikiwa kuwazima kabisa washambuliaji Diego Costa na Pedro Rodriguez wa Chelsea.



Comments