IMEBAINIKA kuwa, huenda Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson angeendelea kuinoa klabu hiyo kama kusingetokea kifo cha mdogo wa mke wake.
Ferguson (73), alistaafu mwaka 2013 akishinda mataji 13 ya Ligi Kuu ya Engoland (EPL) akiwa na klabu hiyo.
Manchester United imeendelea kuwa katika hali ngumu tangu alipoachiwa mikoba David Moyes na sasa Louis van Gaal.
Moyes alitimuliwa miezi 10 baadaye, baada ya kushindwa kutwaa taji la EPL.
Ferguson alisema kuwa, kifo cha Cathy Ferguson mwaka 2012 kilibadilisha kila kitu katika familia yake.
Kocha huyo alisisitiza kuwa ilikuwa vigumu kuendelea kufanya kazi Old Trafford kwani familia hiyo ilimtaka astafu tangu mwaka 2002.
Aidha kocha huyo yupo mbio kuzindua kitabu chake kipya 'Art of Management' kikitokana na uzoefu wake katika soka akiwamo mchezaji Cristiano Ronaldo ambaye aliitumikia klabu hiyo mwaka 2003-2009.
Comments
Post a Comment