SIO LEWANDOWSKI PEKEE, TAZAMA WANAUME WENGINE WALIOTUPIA MAGOLI 5 KATIKA MECHI MOJA


SIO LEWANDOWSKI PEKEE, TAZAMA WANAUME WENGINE WALIOTUPIA MAGOLI 5 KATIKA MECHI MOJA

RobertNa Salym Juma
Nikiwa naamini hali yako ni njema, mimi pia ni mzima kiasi ila nasikitika yanayotokea pale Saudia huku nikiwaombea Marehemu wote wawe salama huko waliko. Tukirejea katika soka, naamini habari ya mujini ni Lewandowski hasa baada ya kufunga magoli 5 pale timu yake ya Bayern Munich ilipo toa kisago cha 5-1 dhidi ya timu ngumu ya Wolfsburg. Kutokana na hili leo nimekuwekea listi ya Wachezaji wengine ambao wamewahi kufunga magoli 5 katika mechi 1, karibu sana kuungana na mimi hapa chini…

ROBERT LEWANDOWSK

Huyu jamaa ni mchezaji hatari sana ambaye kufunga goli inawezekana ndiyo kazi rahisi kuliko hata kuvuta pumzi. Aliwahi kuwafunga Real Madrid magoli 4 kwenye UEFA na hapo dunia ya soka ikaamini kuwa huyu jamaa anaweza kutoa dozi kubwa zaidi endapo atapewa upenyo wa kufanya hivvo. Baada ya Wolfsburg kujichanganya kwenye mechi ya Bundesliga siku kadhaa zilizopita, Lewandowski alitupia magoli 5 peke yake tena ndani ya dakika 9 huku akikamilisha 'hat trick' yake ndani ya dakika 3 na sekunde 22. Kumbuka aliyafanya haya baada ya kutokea benchi huku Bayern ikiwa nyuma kwa goli moja.

LUIZ ADRIANO

luiz-adrianoNi kijana mdogo ambaye hivi karibuni aliandika rekodi ya kufunga magoli 5 katika mechi 1 ya UEFA. FC BATE Borisov ilimruhusu Adriano kufunga magoli 5 mwaka 2014 wakati Shakhtar Donetsk ilipocheza na timu hii na kushinda magoli 7 huku Mbarizil huyu akitupia magoli 5 kwenye usiku wa UEFA na kuandikwa kwenye vitabu vya historia sambamba na mchezaji bora wa Ulaya Lionel Messi ambaye tayari alishawahi kufanya hivi kipindi cha nyuma. Luiz Adriano licha ya kufunga magoli haya, hakufanikiwa kuwa mfungaji bora wa Ulaya kwa kipindi cha 2014.

MIROSLAV KLOSE

Miroslav-KloseNi Mchezaji mwenye busara sana ila Bologna hawatamsahau mwaka 2013 pale ambapo Klose alifunga magoli 5 katika ushindi wa 6-0 walioupata Lazio kwenye mechi ya ligi kuu ya Italia. Klose ni mmaliziaji mzuri sana japokuwa hakujaaliwa chenga wala mbio ila amepewa macho ya ziada ya kutambua nyavu zilipo. Hadi sasa Klose anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kumpiku nguli wa soka Ronaldo de Lima.

FERNANDO MORIENTES

MorientesNaamini Liverpool wanamfahamu vyema kwani ameshacheza Anflied na kushindwa kuwika kama alivyokuwa Hispania. Las Palmas walifungwa 7-0 na Real Madrid mwaka 2002 huku Morientes akitia kambani magoli 5 na kuwa miongoni mwa Wanasoka waliocheza Madrid na kutupia magoli 5 katika mechi 1. Katika mechi hii nakumbuka Morientes alikosa nafasi ya kutupia magoli 6 baada ya kukosa mkwaju wa penati.

ALAN SHEARER

alan shearer

Hakuna asiyefahamu makubwa aliyofanya huyu jamaa katika ligi kuu ya Uingereza. Mwaka 1999, Newcastle iliinyuka Sheffield Wednesday 8-0 huku Shearer akiingia nyavuni mara 5. Japokuwa alifunga penati 2 katika magoli yake ila hadi sasa Shearer anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote katika ligi kuu ya Uingereza na timu yake ya Newcastle.

OLEG SALENKO

5 Jul 1994: HRISTO STOITCHKOV OF BULGARIA CELEBRATES              THE FIRST GOAL DURING THE FIRST HALF OF THE SECOND ROUND              1994 WORLD CUP MATCH AGAINST MEXICO AT GIANTS STADIUM IN              EAST RUTHERFORD, NEW JERSEY.

Japokuwa wengine tulikuwa kwenye 'Mabeseni' ila Ulimwengu wa digitali unatuwezesha kumfahamu huyu jamaa zaidi. Salenko aliwafunga Waafrika magoli 5 baada ya Urusi kuibamiza Cameroon magoli 6-1 kwenye michuano ya kombe la dunia pale Marekani. Hadi sasa rekodi hii haijavunjwa katika michuano hii licha ya miaka 20 kupita tangu Mshambuliaji huyu kufanya unyama huu kwa Waafrika na kuidhihirishia Dunia kuwa Afrika kisoka bado sana. Kutokana na magoli yake, Salenko alifanikiwa kuwa mfungaji bora wa michuano hii ambayo Brazil ilifanya makubwa.

JERMAIN DEFOE

DefoeAkiwa katika ubora wake mwaka 2009, Defoe alitupia magoli 5 pale timu yake ya Spurs iliposhinda 9-1 dhidi ya Dearby Country. Defoe alicheza kwa mafanikio ya wastani katika timu ya Spurs kitu ambacho kilimsaidia kuweka rekodi hii ya kiume ambayo kila mchezaji anatamani kuitekeleza kabla hajastaafu.

LIONEL MESSI

lionel-messi-barcelona-la-liga3248555-1425893997-2343424Alifanya makubwa kwenye usiku wa Uefa mwaka 2012 pale ambapo wachezaji wa Bayer Leverkusen walipompa uhuru na kusahau makali ya mchezaji huyu ambaye inasadikika ndiye bora kuwahi kutokea hapa Duniani. Barcelona iliiadhibu Leverkusen magoli 7-1 kwenye mzunguko wa pili wa hatua ya 16 bora huku Mchawi Messi akimpa kazi mlinda mlango wa Leverkusen kuokota mipira mara 5. Kutokana na magoli haya, Messi alikuwa Mchezaji wa kwanza kufunga magoli 5 katika mechi moja ya UEFA.

RADAMEL FALCAO

Falcao 2Anabezwa sana kwa sasa ila ni Mchezaji aliyeweka rekodi nyingi wakati akiwa katika ubora wake. Ikumbukwe Mwaka 2012 akiwa Atletco de Madrid, Falcao aliwafunga Deportivo la Coruna magoli 5 pale ambapo 'Superdepo' walilala 6-1 kwenye La liga. Falcao alikuwa mchezaji hatari ambaye anawaumiza akili mabeki wa timu pinzani kutokana na utaalamu wake wa kufumania nyavu. Kwa sasa yupo Chelsea na bado anadharaulika kutokana na kushuka kiwango.

DIMITAR BERBATOV

Dimitar BerbatovBaada ya kuondoka Spurs na kwenda United, hatimaye Mchezaji huyu akiwa Old Trafford alitupia magoli 5 pale ambapo United iliinyuka Blackburn Rovers magoli 7-1. Mbulgaria huyu hakupata mafanikio sana akiwa na uzi mwekundu wa United licha ya kufahamika kama miongoni mwa wamaliziaji wazuri hadi sasa licha ya umri wake kusogea.

CRISTIANO RONALDO

ronaldoHuyu jamaa mimi namuheshimu na kumuogopa sana kwani anaamua afunge magoli mangapi katika mechi gani. Cr7 ana uwezo wa kufunga idadi yoyote ya magoli atakayo. Miezi michache iliyopita Madrid ilishinda 9-1 dhidi ya Granada huku Cr7 akiingia nyavuni mara 5 na kuendelea kuandika rekodi mbalimbali ikiwemo ile ya kufunga 'hat-trick' ndani ya dakika 18. Ronaldo ni mchezaji hatari ambaye kwa sasa anainyemelea rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote pale Real
Madrid.

Saijuzedoctor@gmail.com



Comments