SIMBA KAPAKATWA, YANGA NOMA …Tambwe na Busungu wapekeka kilio Msimbazi



SIMBA KAPAKATWA, YANGA NOMA …Tambwe na Busungu wapekeka kilio Msimbazi

Yanga ambayo haijaifunga Simba tangu mwaka 2013, imeibuka shujaa katika mechi ya watani wa jadi kwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ilitawala mchezo kwa kiasi kikubwa lakini Yanga wakawa makini kutumia nafasi chache walizozipata.

Balimi Busungu aliyeingia katikati ya kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Simon Msuva, ndiye aliyebadili sura ya mchezo kwa kuchangia bao la kwanza lililofungwa na Amis Tambwe dakika ya 45.
Kama vile hiyo haitoshi, Busungu akapachika bao la pili kipindi cha pili akitumia vizuri makosa ya mabeki wa Simba.

Mchezo huo ulitawaliwa na kadi nyingi za njano ambazo zilipelekea Mbuyu Twitte  kulambwa kadi nyekundu dakika ya mwisho wa mchezo.


Comments