“SIDHANI KAMA MANCHESTER WATASHINDA LIGI MWAKA HUU”..NANI KASEMA HIVI NA KWANINI



"SIDHANI KAMA MANCHESTER WATASHINDA LIGI MWAKA HUU"..NANI KASEMA HIVI NA KWANINI

Capture

Jana Manchester United wameshinda kwa magoli 3-1 dhidi ya Liverpool na kuendeleza harakati zake kutaka kushinda ligi msimu huu. Lakini Rio Ferdiand haamini kama Man United itashinda ligi kwa msimu huu.

Rio alijunga Man united kwa £32million in 2002 na kuwa mchezaji muhimu wa club hiyo. Huyu jamaa anasema hivi, "Mambo yamebadilika kabisa hivi sasa. mimi nilivyojiunga na Manchester kulikua na club kama Real Madrid, Barcelona, Roma, Chelsea wote walikua wanatamani niende kwao. Lakini mawazo yangu yote yote yalikua nataka kushinda makombe kabla ya kitu chochote ndio maana nikachagua kuwa chini ya Sir Alex Ferguson. Siku hizi Manchester City, Chelsea zinashindana kupata wachezaji kwa pesa nyingi na wachezaji wenyewe kitu kinachowasukuma ni kwenda kupata pesa nyingi na sio kwenda kushinda makombe."

"Kitu kingine hivi sasa Manchester sio kama kipindi mimi nilivyokua naingia pale. Naweza kusema nilikua na bahati kwa kuingia changning room na watu kama Roy Keane, David Beckham, Ryan Giggs, Ruud van Nistelrooy, Juan Sebastian Veron. Sio mimi mpya nilikua nategemewa kutoa mchango mkubwa kwa timu lakini hao niliowakuta ndio walikua tegemezi kwa timu. Tofauti na sasa hivi kuona mtu kama Martial au Depay ndio wajiunga na Manchester, harafu wao ndio wanategemewa kufanya maajabu na sio wakina Rooney au Michael Carrick ambao ndio msingi wa club"

"Kimsingi labda Manchester inaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya ushindani wa kushinda ligi kama hawa vijana wapya wakizoea ligi mapema na kufunga magoli mengi. Labda itasaidia lakini wakishindwa kuzoea EPL mapema sioni matumaini kwa Manchester united"

2C24819B00000578-3232209-image-m-41_1442090581118



Comments