SHARAPOVA KUREJEA ULINGONI SEPTEMBA 27



SHARAPOVA KUREJEA ULINGONI SEPTEMBA 27

MCHEZAJI namba moja wa zamani katika medani ya tenisi duniani Maria Sharapova anatarajiwa kurudi katika uga wa mchezo huo kwenye michuano ya wazi ya Wuhan Open itakayoanza Septemba 27 mwaka huu.

Michuano hiyo itakayochezwa nchini China itamrudisha nyota huyo dimbani baada ya kupata maumivu ya goti yaliyomfanya akose Wimbledon na US Open mwaka huu.

Sharapova,28, raia wa Russia na bingwa mara tano wa Grand Slam alikaririwa akisema "Ni wakati muhimu kwangu kurudi tena katika Michuano ya Wazi ya Wuhan kwani nimekuwa nikifanya mazoezi kwa bidii kwa ajili ya kurudi dimbani nikiwa fiti," alisema nyota huyo.



Comments