SERGIO AGUERO, KEVIN DE BRUYNE NA RAHEEM STERLING WAONGOZA MAANGAMIZI YA MAN CITY DHIDI YA SUNDERLAND
Kama kuna kipimo chochote kilichohitajika kuangalia uwezo wa timu iliyopo kileleni mwa Premier League na ile inayoburuta mkia, basi mechi hii ni kipimo halisi.
Vinara wa Ligi Kuu Manchester City wakaumana na Sunderland iliyopo mkiani katika mchezo wa upande mmoja wa Capital One na kushuhudia kipigo cha bao 4-1 Sunderland wakilala katika uwanja wao wa nyumbani Stadium of Light.
Ilikuwa ni kama kukumbushia fainali ya kombe hilo ya mwaka 2014 pale timu hizo zilipokutana ambapo Sunderland waliongoza hadi mapumziko lakini mwisho wa siku walala 3-1.
Lakini safari hii City wakamaliza biashara mapema na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 4-0 kupitia kwa Sergio Aguero aliyefunga kwa penalti dakika ya 9, Kevin de Bruyne dakika ya 25, bao la kujifunga la kipa Vito Mannone dakika ya 33 na Raheem Sterling aliyekwamisha mpira wavuni dakika ya 36.
Bao pekee la Sunderland lilifungwa dakika ya 83 na Ola Toivonen.
Sergio Aguero akishangilia bao lake aliliofungia Manchester City ndani ya dakika 10 za mwanzo dhidi ya Sunderland katika mchezo wa Capital One
Kevin De Bruyne akiifungia Manchester City bao la pili
De Bruyne aliyesajiliwa kwa bei mbaya kutoka Wolfsburg kiangazi hiki akishangilia bao lake dhidi ya Sunderland katika uwanja wa Stadium of Light
De Bruyne mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji akipongezwa na wachezaji wenzake wa Manchester City Raheem Sterling na Jesus Navas
Comments
Post a Comment