RUUD VA NISTELROOY ATAKA ROONEY AWE MPISHI WA ANTHONY MARTIAL


RUUD VA NISTELROOY ATAKA ROONEY AWE MPISHI WA ANTHONY MARTIAL

NYOTA wa zamani wa Manchester United Ruud va Nistelrooy amesisitiza kuwa, chipukizi Anthony Martial (pichani) atapendeza sana akiongoza mashambulizi huku Rooney akisimama kama mshambuliaji wa pili katika Klabu hiyo.

Mfaransa huyo, 19, alitua Manchester United kwa kitita cha pauni mil. 36 akitoka Monaco ambapo siku chache zilizopita katika mtanange dhidi ya Liverpool alifunga bao.

Nistelrooy alikaririwa akisema; "Anaonekana kama mshambuliaji anayeweza kufunga mabao badala ya kuwafanyia wengine kazi."

Nyota huyo wa Uholanzi aliongeza kuwa Wayne Rooney ndiye anafaa kufanya zaidi kazi kwa safu ya ushambuliaji kwani ana nguvu na akili ya kutosha.

Martial alicheza katika mtanange wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya PSV ambao ulimazika kwa Manchester United kutandika mabao 2-1.

Rooney atarudi dimbani juma hili katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL) dhidi ya  Southampton baada ya kupata majeruha wiki iliyopita.

Nistelrooy alipokuwa Manchester United (2001-2006) alifunga mabao 150 katika mechi 219 alizocheza.




Comments