RONALDO ATAKA KUCHEZA TENA NA WAYNE ROONEY


RONALDO ATAKA KUCHEZA TENA NA WAYNE ROONEY

Cristiano Ronaldo and Wayne RooneyMchezaji Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, amefunguka na kudai kuwa amemiss kucheza na nahodha wa Manchester United Wayne Rooney.

Ronaldo ameyasema hayo weekend hii katika documentary yake ambayo ameeleza jinsi alivyoimiss klabu yake ya zamani Manchester United, huku akitaka kucheza na Rooney kwa mara nyingine tena.

Akimwagia sifa Rooney, Ronaldo amesema wazi kuwa nahodha huyo wa United ni moja kati ya wachezaji wakubwa duniani, lakini pia ni kijana wa kiingereza anayependwa huku akikumbuka namna alivyomsaidia wakati walipokua pamoja Old Trafford.

Ronaldo aliichezea Manchester United kwa misimu sita, na sasa akiwa katika msimu wake wa sita pia na Real Madrid taarifa zinasema huenda ukawa ndio msimu wake wa mwisho Bernabeu.

Manchester United watakua na nafasi kubwa ya kumnasa Ronaldo endapo watamhitaji kwakua taarifa zinasema Real Madrid watakua tayari kumuachia na kupata pesa mwishoni mwa msimu huu.

Ronaldo na Rooney waliunda combination nzuri na hatari zaidi Old Trafford na kufanikiwa kutwaa mataji kadhaa ya nyumbani na klabu bingwa Ulaya.



Comments