Winga wa Raeal Madrid Cristiano Ronaldo amefunga goli tatu (hat-trick) katika ushindi wa oli 4-0 iliopata klabu yake dhidi ya Shakhtar Donetsk kwenye mchezo mwingine wa kundi A wa michuano ya kbabu bingwa Ulaya uliopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu.
Ronaldo amefunga magoli hayo dakika ya 55 kwa mkwaju wa penati, akafunga goli jingine kwa mkwaju wa penati pia ikiwa ni dakika ya 63 na akahitimisha hat-trick yake dakika ya 81.
Karim Benzema alifunga goli la kwanza dakika ya 30 kipindi cha kwanza kabla ya Ronaldo kuzama kambani mara tatu hatimaye kuondoka na mpira mara baada ya mchezo kumalizika.
Comments
Post a Comment