Huku Bayern Munich ikiwa nyumba kwa bao 1-0 dhidi ya Wolfsburg hadi mapumziko, Robert Lewandowski akaingizwa kipindi cha pili na kufunga magoli matano ndani ya dakika 9.
Mabingwa hao watetezi wa Bundesliga, waliingia kuvaana na washindi wa pili wa msimu uliopita wakiwa na rekodi ya ushindi wa asilimia 100 tangu msimu mpya uanze, lakini wakajikuta wakiwa nyuma kwa bao la kipindi cha kwanza kutoka kwa Daniel Caligiuri hali iliyomlazimisha kocha Pep Guardiola kufanya mabadiliko wakati wa mapumziko.
Kocha huyo wa Bayern akamtoa kiungo Thiago Alcántara na kumwingiza mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Poland ambaye akaenda kuleta mafuriko ya magoli.
Hiyo ni rekodi mpya ya magoli ya haraka haraka katika Bundesliga.
Lewandowski angeweza kufunga magoli mengi zaidi kama sio shuti lake moja kugonga mwamba na lingine kuokolewa na kipa Diego Benalgio.
Robert Lewandowski akishangilia bao lake la tano dhidi ya Wolfsburg
Lewandowski akiisawazishia Bayern Munich
Lewandowski akiserereka kushangilia bao lake la pili
Ubao wa matokeao ukionyesha namna magoli yalivyomiminika
Comments
Post a Comment