PLUIJM: “HATUWAOGOPI SIMBA…”


PLUIJM: "HATUWAOGOPI SIMBA…"
Hans van der Pluijm, kocha mkuu wa klabu ya Yanga

Hans van der Pluijm, kocha mkuu wa klabu ya Yanga"

Kocha mkuu wa timu ya Yanga mholanzi Hans van der Pluijm amesema, timu yake imepata ushindi kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu kutokana na yeye kumfahamu vyema kocha wa imu hiyo na aina ya soka wanalotumia wapinzani wao.

Kuelekea mchezo wao wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Simba, Pluijm amesema watajiandaa na mchezo huo kama wanavyojiandaa na michezo mingine kwasababu mchezo huo hauna tofauti na michezo mingine ila unakuwa na mashabiki wengi.

"Tumeshinda mechi tatu hadi sasa, ukiangalia utaona kuna mabadiliko kwenye timu, dakika 25 za kwanza hatukuchea mpira wenye presha kubwa tulijadiliana kuhusu makosa tuliyokuwa tukifanya kwenye mechi zilizopita na jinsi ya kuzuia kurudia makosa hayo".

"Timu ya JKT Ruvu haikucheza vizuri na sisi tulichukua udhaifu huo kama faida kwetu na tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga hasa dakika 20 za mwisho".

"Tumecheza na Ruvu ambayo namfahamu kocha wake na mbinu zake, kwahiyo ukicheza na timu mbayo unamfahamu kocha wake na tabia zake hawataweza kukusumbua na hakutakuwa na kitu kipya kutoka kwao".

"Unapocheza na timu inayotumia nguvu nyingi inabidi ucheze mpira wa haraka na kasi kubwa ili umiliki mpira kwa kiasi kikubwa, nimefurahi kupata ushindi lakini bado tunatakiwa kufanyia kazi baadhi ya mapungufu".

"Mechi yetu dhidi ya Simba ni sawa na mechi nyingine tu lakini mechi hiyo inatawaliwa na mashabiki. Ni sawa na vita, usipomuua adui yako anakuua wewe. Kwa upande wangu mimi, tutajiandaa kama tunavyojiandaa kwa ajili ya mechi nyingine kwasababu naamini tutacheza mpira".

"Hatuiogopi Simba hicho ndicho naweza kukwambia, tunawaheshimu wapinzani wetu wote na hicho ndicho tunatakiwa kufanya lakini hakuna timu tunayoiogopa".



Comments