Kiongozi wa kikundi cha ushangiliaji cha timu ya Kauzu FC Juma Ally maarufu kama 'Ostadh' amewashukuru wadhamini wa michuano hiyo baada ya kupokea shilingi milioni moja (1,000,000) kama zawadi ya kikundi bora cha ushangiliaji na kuahidi kuwa wanajipanga kwa ajili ya michuano ya msimu ujao ambayo.
"Nashukuru sana kupata zawadi hii ya ushangiliaji bora na najua kwamba pesa hii si ya kwangu pekeangu bali ni ya kundi zima, ntakachokifanya ni kwenda kuwaambia wenzangu kwamba tumepata zawadi ya kikundi bora cha ushangiliaji na msimu ujao tujipange vizuri zaidi ya mwaka huu", Ostadh alishukuru.
"Pesa hii tutachua semu kidogo kwa ajili ya kupongezana halafu nyingine tunakwenda kuifungulia account kwasababu mwakani kama Mungu akipenda tutashiriki tena kwa hiyo itakuwa ikitusaidia kwa kununulia vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya kikundi cha ushangiliaji".
Comments
Post a Comment