ORODHA YA TIMU 5 ZENYE KADI NYINGI NYEKUNDU KWENYE HISTORIA YA EPL


ORODHA YA TIMU 5 ZENYE KADI NYINGI NYEKUNDU KWENYE HISTORIA YA EPL

Arsenal-red-cardArsenal ilipata kadi mbili nyekundu kwenye mchezo wake wa mwisho ilipoangukia pua kwa kichapo cha goli 2-0 mbele ya Chelsea. Kwa ujumla Arsenal wameshaoneshwa kadi nyekundu 79 kwe historia ya ligi ya England (EPL).

Baada ya kadi nyekundu iliyozua utata aliyooneshwa Gabriel Paulista, hapa kuna orodha ya vilabu vitano ambavyo wachezaji wake wameoneshwa kadi nyekundu nyingi zaidi kwenye historia ya EPL.

5. Chelsea FC-Kadi nyekundu 71

West Bromwich Albion v Chelsea - Premier LeagueChelsea ni mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu nchini England, wameshinda taji hilo mara nne kwenye historia ya klabu hiyo. Wao wanashikilia nafasi ya tano kwenye orodha ya timu ambazo wachezaji wake wameoneshwa kadi nyingi kwenye historia ya EPL.

4. Newcastle United-Kadi nyekundu 75

FBL-ENG-PR-MAN CITY-NEWCASTLETangu walipopanda daraja kucheza ligi kuu ya England msimu wa 1993/94, Newcastle imepata kadi nyekundu 75 na kwenye orodha hii wanakamatia nafasi ya nne.

3. Blackburn Rovers-Kadi nyekundu 76

Blackburn red cardBlackburn ilikuwa kwenye ligi ya EPL tangu mwaka 1992 lakini ilishuka daraja kati ya mwaka 1999 na 2001. Wakapanda tena msimu wa 2001/02. Kwa bahati mbaya, Blackburn wakashuka tena miaka 11 baadae. Tangu 2012 Blackburn wanacheza ligi daraja la kwanza (Championship). Wakati wakiwa ligi kuu, walioneshwa kadi nyekundu mara 76.

2. Arsenal-Kadi nyekundu 79

Arsenal red cardArsena haijawahi kushuka daraja tangu English Division One ilipoanza kuitwa Premier League msimu wa 1992/93. Patrick Vieira ndie mchezaji anaeshikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyeoneshwa kadi nyekundu mara nyingi kwenye historia ya ligi hiyo. Alikuwa ni mchezaji wa Arsenal kati ya 1996 na 2005. Alioneshwa kadi nyekundu mara nane (8) wakati akicheza kwenye ligi hiyo.

1. Everton FC-Kadi nyekundu 80

Everton red cardEverton ndiyo klabu iliyooneshwa kadi nyekundu mara nyingi kwenye ligi ya England. Duncan Ferguson alicheza Everton kati ya 1994 na 1998 na baadae kati ya 2000 na 2006. Alishuhudia akioneshwa kadi nyekundu mara nane kwenye historia yake ya soka nchini humo.



Comments