NINI KIMEWASIBU WAKALI HAWA WA KUCHEKA NA NYAVU?



NINI KIMEWASIBU WAKALI HAWA WA KUCHEKA NA NYAVU?

Floppy 5Sergio Aguero, Harry Kane, Diego Costa, Alexis Sanchez, Eden Hazard na Wayne Rooney ni wa achezaji sita waliofunga jumla ya magoli 109 kwa pamoja msimu uliopita kwenye ligi kuu ya soka nchini England (EPL) lakini wote wameshindwa kutamba msimu huu katika mechi ambazo tayari wameshacheza.

Mechi sita ambazo tayari wamecheza kwenye msimu huu washambuliaji hao wamejikuta wakifunga magoli matatu ukijumuisha idadi ya mechi zote walizocheza hazipungui 35 wakati huo goli moja la Eden Hazard linatazamwa kama Calum Chambers alijifunga.

Washambuliaji wa kati Kane (Tottenham), Aguero (Manchester City) and Costa (Chelsea) walikuwa kwenye top three ya wafungaji kwenye EPL msimu uliopita.

Sanchez (Arsenal), Hazard (Chelsea) and Rooney (Man United) walikuwa wakitokea pembeni na wote walichangia upatikanaji wa baadhi ya magoli. Rooney aliweka historia ya kuwa mfungaji wa muda wote wa England mwezi huu lakini akiwa amefunga magoli manne pekee mwaka 2015.

Washambuliaji hao wanahitaji kujiamini. Hali hiyo inaweza ikaondoka bila sababu yoyote na kuchukua muda kurejea. Au inaweza kusababishwa na mambo tofauti kama vile umri, malengo au wakati mwingine vyote kwa pamoja.

Makocha wanasema huenda hali hiyo inasababishwa na mchoko (kucheza mfululizo). Wachezaji ambao hata wao hawahisi kuchoka lakini wanaambiwa wamechoka. Kane, Aguero and Sanchez wote walikuwa kwenye mashindano wakati ligi ikiwa kwenye mapumziko.

Kane alirejea nyumbani akitokea kwenye michuano ya mataifa ya Ulaya U21. Aguero (Argentina) na Sanchez (Chile) walicheza fainali ya Copa America Julai 4. Hawakuwepo kwenye ziara za klabu zao za kujianndaa na msimu mpya, walianzia benchi kwenye mechi za kwanza za msimu mpya.

Aguero ametumia muda mchache uwanjani ukilinganisha na wenzake sita lakini amecheza mechi za kirafiki za kimataifa mapema mwezi huu nchini Marekani, wakati Sanchez alikuwa Chile kwenye mechi dhidi ya Paraguay.

Costa, Sanchez na Kane walikuwa ni wachezaji wapya kwenye ligi ya England msimu uliopita na walifanya kazi kwa bidii sana. Walitumia muda mwingi kuwasoma wapinzani wao ili kuhakikisha wanafunga magoli.

Katika orodha ya wafungaji bora watano, wanne walikuwa ni wageni wa ligi hiyo; Kane, Costa, Sanchez pamoja na Charlie Austin Aguero pekee ndiye hakuwa mgeni wa ligi hiyo.

Asilimia  25 ya mashuti aliyopiga Aguero kwenye mechi sita za mwanzo msimu uliopita alifunga, lakini msimu huu ni asilimia 6.7.

Sergio Aguero

FloppyMechi sita za kwanza: 2014-15

Mashuti 16 magoli 6

Mechi sita za kwanza: 2015-16

Mashuti 15 goli 1

Harry Kane

Floppy 1514 ni namba za dakika ambazo mshambuliaji huyo wa England amecheza msimumhuu bila kufunga goli. Msimu uliopita alikuwa na wastani wa kufunga kila baada ya dakika 95.

Wayne Rooney

Floppy 2Rooney ameshindwa kufunga kwenye mashuti saba aliyopiga msimu huu 2015-16, alifunga mabao matatu kwenye kila mashuti 12 aliyopiga kwenye mechi sita za kwanza msimu uliopita.

Mechi sita za kwanza: 2014-15

Mashuti 12 magoli 3

Mechi sita za kwanza:2015-16

Mashuti 7 magoli 0

Eden Hazard

Floppy 3Mbelgiji huyo wastani wake wa kupiga mashuti umeshuka msimu huu kwa mechi sita alizocheza mpaka sasa ukilinganisha na ilivyokuwa 2014-15.

Mechi sita za kwanza: 2014-15

Asilimia 80 ya mashuti yake yalilenga goli huku yalioyokwenda nje ya lango yakiwa ni asilimia 20.

Mechi sita za kwanza 2015-16

Asilimia 50 ya mashuti yamelenga goli na asilimia 50 yameenda nje ya goli.

Diego Costa

Floppy 6Mechi sita za kwanza:2014-15

Mechi sita magoli 8

Mechi sita za kwanza:2015-16

Mechi sita goli 1

Floppy 4



Comments