Mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Ufaransa Nicolas Anelka anaamini kinda hatari wa Manchester United Anthony Martial atakuwa tishio huku akimtaja kuwa ni moja ya wachezaji bora wanaochipukia katika kizazi cha sasa.
Anthony Martial ambaye amekuwa akifaninishwa na Thierry Henry na Anelka, amekuwa gumzo tangu Manchester United ilipomsajili kutoka Monaco kwa pauni milioni 36 kiangazi hiki.
Ada yake inaweza ikapanda hadi pauni milioni 58 kutegemea na maendeleo yake na tayari mshambuliaji huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Ufaransa ameanza kujenga himaya yake katika Premier League.
Akiongea na mtandao wa kimataifa wa Goal.com, Anelka alisisitiza kuwa hashangazwi na mafanikio ya haraka ya Maritial ndani ya Manchester United.
"Anthony ni mchezaji mzuri sana na nina uhakika ataifanyia makubwa United," alieleza Anelka kwenye umri wa miaka 36.
Anthony Martial ni mmoja wa wachezaji bora wa kizazi hiki, hiyo ni kwa mujibu wa Nicolas Anelka
Anelka (kulia) anaamini Martial atafanya makubwa
Comments
Post a Comment