LEO ni miaka minne toka kifo cha mmoja wa watunzi na waimbaji bora waliowahi kutokea kataika muziki wa dansi Tanzania, Selemani Kasaloo Kyanga ambae alizikwa katika makaburi ya Sinza . Kasaloo alikuwa ni pacha wa nduguye Kyanga Songa ambae nae ni marehemu, walizaliwa nchini Kongo 1957. Mapacha hawa waliofanana walikuwa nyota katika kila bendi waliyopigia, kati ya bendi walizopigia wakiwa nchini ni Matimila, Makassy, Maquis, Sambulumaa, Ngorongoro Heroes, Tancut Almasi, Kalunde Band na Sandton Sound. Kasaloo atakumbukwa katika nyimbo nyingi zinazoendelea kutamba mpaka leo kama vile Kalubandika, Masafa Marefu, Nimemkaribisha nyoka
Mungu Amlaze pema Seleman Kasaloo Kyanga (Mwanakaa).
Kasaloo akiwa Tancut Almasi, toka kushoto Buhero Bakari,Abdul Salvador, Kasaloo, Asha Salvador, Kyanga Songa
Comments
Post a Comment