MWAMUZI BORA NDONDO CUP AELEZEA MECHI NGUMU KUWAHI KUKUTANA NAYO KWENYE MAISHA YAKE YA SOKA



MWAMUZI BORA NDONDO CUP AELEZEA MECHI NGUMU KUWAHI KUKUTANA NAYO KWENYE MAISHA YAKE YA SOKA
Jackson Msilombo akizungumza mara baada ya kukabidhiwa              zawadi ya shilingi laki tano kama mwamuzi bora wa michuano              ya Dr. Mwaka Sports Xtra Ndondo Cup 2015

Jackson Msilombo akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya shilingi laki tano kama mwamuzi bora wa michuano ya Dr. Mwaka Sports Xtra Ndondo Cup 2015

Jackson Msilombo ameibuka kuwa mwamuzi bora wa michuano ya Dr. Mwaka Sports Xtra Ndondo Cup msimu huu na kufanikiwa kutwaa kitita cha shilingi laki tano kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo.

Msilombo amesema jitihada zake binafsi, kusoma sana sheria za mchezo huo, kufanya mazoezi ya kutosha na kupata mechi nyingi za kuchezesha ndio kumemfanya yeye kufanya vizuri hatimaye kuibuka refa bora wa mashindano ya Ndondo Cup msimu huu.

"Jitihada zangu mwenyewe ambazo huwa nazifanya nafanya sana mazoezi na kusoma sheria, pia huwa najifunza kwa wenzangu kupitiaushauri na kikubwa ni kupata michezo mingi sana", amesema Msilombo.

"Mechi ya fainali ya Ndondo kwangu ilikuwa kubwa sana kwasababu ni mechi inayooneshwa moja kwa moja (live) halafu ilikuwa na mashabiki wengi sio tu uwanjani bali hata majumbani watu wengi sana walikuwa wanaifatilia mechi ile".

"Nilifanya maandalizi siku mbili kabla ya mchezo kwa kusoma sana sheria ili siku nitakayokuwa mchezoni nisifanye makosa".

"Nimekutana na matukio mengi kwenye soka tangu nianze kuchezesha mpira lakini mambo mengi yanatokana na watu kuzosoma sheria lakini sisi tunazitafsiri sheria hizo nah ii inaleta maneo mengi sana".



Comments