MOURINHO ASHIKIWA PABAYA URENO, CHELSEA YALALA 2-1 KWA PORTO ...Maccabi Tel Aviv yachapwa 2-0 na Dynamo Kyiv
Jose Mourinho amerejea vibaya kwenye timu yake ya zamani - Porto ya Ureno baada ya Chelsea kutandikwa bao 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Hadi mapumziko timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 1-1 ambapo Porto walikuwa wa kwanza kufunga dakika ya 39 kupitia kwa Andre Andre huku Willian akiisawazishia Chelsea dakika ya 45.
Dakika ya 52 Porto wakafunga bao la ushindi kupitia kwa Maicon.
Katika mchezo mwingine wa kundi G, Maccabi Tel Aviv ikiwa nyumbani ikalala 2-0 kwa Dynamo Kyiv.
PORTO (4-1-4-1): Casillas 6; Pereira 6, Maicon 7, Marcano 6.5, Indi 6.5 ; Danilo 6; Andre 7.5 (Layun 80), Neves 7 (Evandro 78), Imbula 7.5, Brahimi 8 (Osvaldo 87); Aboubakar 7
CHELSEA (4-2-3-1): Begovic 7; Ivanovic 4.5, Zouma 5.5, Cahill 6, Azpilicueta 6; Ramires 6 (Matic 73, 5), Mikel 6 (Hazard 62, 5); Pedro 5 (Kenedy 73, 5), Fabregas 5, Willian 6.5; Costa 6
Maicon wa Porto akishangilia bao la ushindi dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Dragao Stadium
Andre Andre akishangilia bao la kwanza
Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Willian akiteleza kwa furaha baada ya kuifungia Chelsea bao la kusawazisha
Cesc Fabregas (kulia) na Diego Costa (katikati) wakiwa hoi baada ya Maicon (kushoto) kufunga bao la pili
Comments
Post a Comment