Jose Mourinho amethibitisha kuwa mlinda mlango namba moja Thibaut Courtois atafanyiwa upasuaji wa goti na atakuwa nje ya dimba kwa muda mrefu.
Thibaut Courtois aliumia goti akiwa mazoezini mapema wiki hii na sasa Chelsea itaanza kukosa huduma yake kuanzia mechi ya Jumamosi hii dhidi ya Everton.
Hata hivyo Mourinho amejipa moyo na kusema kipa Asmir Begovic aliyesajiliwa kutoka Stoke City kiangazi hiki, ataziba pengo hilo bila wasiwasi.
Mourinho amesema: "Kila mtu alirejea salama kutoka kwenye mechi za kimataifa, lakini Courtois akaumia mazoezini na atakosekana kwa muda mrefu."
Jose Mourinho akithibitisha kuwa Thibaut Courtois atakuwa benchi kwa muda mrefu
Comments
Post a Comment