KOCHA Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa, bado kikosi chao kinatakiwa kufanyiwa marekebisho katika sehemu ya ushambuliaji.
Mkwasa aliyasema hayo alipozungumza na Saluti5 jijini Dar es Salaam, ambapo akafichua kuwa bado wanaendelea kuwanoa washambuliaji wao.
Alisema wamegundua kuwa kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union na Prisons, washambuliaji wao walipoteza nafasi nyingi za kufunga mabao.
"Pamoja na kushinda, lakini bado tuna kasoro kwenye nafasi ya kufunga, tumekuwa tukipoteza nafasi nyingi za kushinda mabao, tunafanyia kazi," alisema.
Mkwasa alisema timu inapotengeneza nafasi zaidi ya tano katika kipindi cha kwanza na kushindwa kuzitumia, ni tatizo na inajiweka kwenye nafasi kubwa ya kupoteza mchezo.
Comments
Post a Comment