Katika mchezo wa jana kati ya Azam FC dhidi ya Tanzania Prisons, jambo la kuvutia ilikuwa ni pale mtandao huu ulipopata nafasi ya kuzunguza na mke wa Serge Pascal Wawa beki wa Azam ambaye amekuwa gumzo siku za hivi karibuni kutokana na uwezo mkubwa ambao amekuwa akiuonesha uwanjani.
Mke wa Wawa anaefahamika kwa jina na Martine Wawa alikuwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo uliokuwa wa ufunguzi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) msimu huu ambapo Azam walicheza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Martine amesema yeye hufurahi sana pale timu anayocheza mumewe inapoibuka na ushindi kwani anaamini mumewe huwa na amani pale timu yake inapopata matokeo mazuri.
"Huwa ninafurahi sana pale timu anayocheza mumewangu inapoibuka na ushindi kwenye mechi wanazo cheza kwani huwa anarudi nyumbani akiwa na amani kuliko pale timu ianapopata matokeo tofauti na alivyokuwa anatarajia".
"Mumewangu huwa anafurahi na anakuwa na amani timu yake inaposhinda, mara kadhaa ambazo nimekuwa nikimshuhudia akicheza uwanjani huwa anajituma sana kuhakikisha timu inashinda. Sasa kama ikitokea wamepoteza mchezo huwa anakosa amani na hii nadhani ni kutokana na jinsi ambavyo huwa anajitolea kwa kila kitu ili washinde".
"Huwa napata wakati mgumu kumrejesha kwenye hali yake ya kawaida endao timu inapata matokeo tofauti na matarajio yake, Wawa ni mtu anaetaka kushinda kila mechi. Sasa matokeo tofauti na hayo huwa yanamuumiza sana na hapo ndipo hurudi nyumbani akiwa hana amani kabisa lakini nashukuru huwa ananielewa napomwambia akubali matokeo na kujipanga upya kwa mechi inayofuata".
Comments
Post a Comment