MINZIRO ATOA SABABU ZA KIPIGO TOKA YANGA




MINZIRO ATOA SABABU ZA KIPIGO TOKA YANGA
Fred Felix Minziro, kocha mkuu wa JKT Ruvu ya mkoani              Pwani

Fred Felix Minziro, kocha mkuu wa JKT Ruvu ya mkoani Pwani

Kocha wa JKT Ruvu Fred Felix Minziro kwa upande wake yeye amewalaumu wachezaji wake kwa kile alichokiita ni uzembe na kutotimiza majukumu aliyowaambia ndiko kumepelekea kupoteza mchezo wao dhidi ya Yanga huku akisema kukosa umakini kwa vijana wake ndiko kulipelekea Yanga kutumia udhaifu huo kupata ushindi.

"Makosa na uzembe wa wa golikipa  umepelekea kufungwa magoli mepesi, sio kila shambulizi ni goli lakini kwetu kila tuliposhambuliwa na Yanga tuliruhusu goli. Yanga wana wacheaji wengi proffesionals kuliko ilivyo kwetu, walituzidi kwa umakini uwanjani. Kwenye mpira ukifanya kosa, adui akitumia nafasi hiyo vizuri anakufunga", amesema Minziro.

"Niliwaandaa wachezaji wangu, nimewapa maagizo yote na majukumu lakini hawajatekeleza ndani ya uwanja. Tatizo kubwa la wachezaji wetu wa kitanzania hawakutokea kwenye 'Academy'" .

"Angalia aina ya magoli tuliyofungwa, angalia umakini wa golikipa golini, angalia tofauti kubwa kati yetu sisi na wenzetu Yanga, utaona kunatofauti kubwa sana wenzetu wana wachezaji 'profesionals' ambao wako makini. Angalia magoli ambayo wametufunga, ukifanya uzembe mchezaji ni goli".

"Tunajipanga kuhakikisha tukirejea nyumbani tunapata ushindi na kupata pointi tatu na sisi kwenye mechi inayofuata".



Comments