Mshambuliaji wa Manchester United Memphis Depay amedhihirisha kuwa yeye ni 'bishororo' wa kutupwa pale alipokwenda kujirusha klabu huku akiwa amepiga pamba za kufa mtu sambamba na meno ya bandia ya dhahabu.
Hiyo ilikuwa ni Jumamosi usiku masaa kadhaa baada ya Manchester United kuitungua Sunderland 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu katika uwanja wa Old Trafford.
Memphis Depay ambaye alitupia wavuni bao moja, akaenda kujirusha Suburbia nightclub kiwanja ambacho alikuwepo pia demu wa zamani wa Chris Brown Karrueche Tran
Memphis Depay akiwa amevaa meno ya bandia ya dhahabu ndani ya Suburbia night club Jumamosi usiku
Depay akishangilia goli lake alilofunga Jumamosi
Depay akiwa mbele ya Karrueche Tran (kulia) demu wa zamani wa Chris Brown
Karrueche Tran (kulia) kipenzi cha zamani cha Chris Brown nae alikuwepo kiwanja alichojirusha Depay
Comments
Post a Comment