MASIKINI MESSI…!! AIPA PIGO BARCELONA



MASIKINI MESSI…!! AIPA PIGO BARCELONA
Lionel Messi akiugulia maumivu baada ya kugongana ana              beki wa Las Palmas Pedro Bigas

Lionel Messi akiugulia maumivu baada ya kugongana ana beki wa Las Palmas Pedro Bigas

Mchezaji wa Barcelona Lionel Messi amepata pigo kubwa kwake mwenyewe na timu yake baada ya kuumia kiungo cha ndani ya goti na katika mchezo wa timu yake ilipoifunga Las Palmas kwa magoli 2-1 jumamosi hii.

Messi ambaye aligongana na mchezaji beki wa Las Palmas, Pedro Bigas katika dakika ya tatu, aliendelea kucheza lakini akashindwa kuendelea nakuomba kufanyiwa mabadiliko katika dakika ya nane ya mchezo.

Baada ya kupelekwa hospitali, imefahamika kuwa atakaa nje ya uwanja kwa takribani week 7-8. Messi ameumia kiungo katika goti lake kitaalam 'collateral ligament tear'.

Kipa wa Las Palmas Javi Varas akijaribu kumuangalia              Messi baada ya kugongana na beki wa timu hiyo Pedro Bigas

Kipa wa Las Palmas Javi Varas akijaribu kumuangalia Messi baada ya kugongana na beki wa timu hiyo Pedro Bigas

Kocha wa Barcelona, Luis Enrique amesema hakuna kitu kibaya kama majeruhi kwa mchezaji, lakini akasema taarifa hizi ni njema kwa wapinzani wao.

Messi alitibiwa maumivu yake mara ya mwisho 2013 na kurudi katika fomu yake vizuri huku akiweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa klabu wa muda wote.



Comments