Manchester United wamezinduka leo baada ya kuitandika Liverpool kwa mabao 3-1, mchezo uliopigwa katika dimbala Old Trafford, maskani kwa Manchester United.
United walipoteza dhidi ya Swansea wiki mbili zilizopita baada ya kufungwa mabao 2-1.
Mabao ya Man united yamefungwa na Daley Blind dakika ya 49, la pili likafungwa na Ander Herrera dakika ya 70 kwa njia ya penati huku la tatu likiwekwa kimiani na kinda aliyenunuliwa hivi karibuni kutoka Monaco kwa ada ya pauni milioni 36 Anthony Martial mnano dakika ya 86.
Kwa upande wa Liverpool, goli lao la pekee lilifungwa na Mbelgiji Christian Benteke dakika ya 84.
Vikosi vilikuwa hivi;
Manchester United: De Gea, Darmian, Smalling, Blind, Shaw, Carrick (Schneiderlin 72), Schweinsteiger, Mata (Martial 65), Herrera, Depay (Young 45), Fellaini
Ambao hawakuingia: Rojo, Romero, Valencia, McNair
Kadi ya njano: Darmian
Magoli: Blind 49, Herrera 70 (pen), Martial 86
Liverpool: Mignolet, Clyne, Skrtel, Lovren, Gomez, Milner, Lucas (Moreno 88), Can, Firmino (Ibe 65), Benteke, Ings (Origi 74)
Wachezaji ambao hawakuingia: K. Toure, Sakho, Bogdan, Rossiter
Goli: Benteke 84
Kadi ya njano: Clyne, Milner
Refarii: Michael Oliver
Mchezaji bora wa mchezo: Daley Blind
Comments
Post a Comment