MANCHESTER UNITED YAONGOZA LIGI KUU KWA MARA YA KWANZA TANGU SIR ALEX FERGUSON AACHIE NGAZI ...Rooney afunga goli lake la kwanza Premier League
Louis van Gaal aliahidi kuipa taji Manchester United ndani ya miaka mitatu lakini sasa ndoto hiyo inaonekana inaweza ikatimia katika mwaka wake pili baada ya timu hiyo kuinyuka Sunderland 3-0.
Katika mchezo huo wa Premier League uliochezwa Jumamosi, United ilipata bao la kwanza kupitia Memphis Depay kunako dakika ya 45 huku Wayne Rooney akifunga bao lake la kwanza Ligi Kuu msimu huu katika dakika ya 46 kabla ya Juan Mata kuifungia klabu hiyo bao la tatu dakika ya 90 kwa shuti kali la karibu.
Rooney hakufunga bao lolote Premier League tangu mwezi April msimu uliopita.
Kwa ushindi huo Manchester United imefanikiwa kuongoza msimamo wa Premier League kwa mara ya kwanza tangu Sir Alex Ferguson alipostaafu kuikochi timu hiyo mwaka 2013.
Licha ya kutokufunga bao katika mchezo huu, mshambuliaji mpya wa Manchester United Anthony Martial ndiye aliyeng'ara zaidi.
Manchester United (4-2-3-1): De Gea 6.5; Valencia 5.5, Smalling 6, Blind 7 (Jones 74 6), Darmian 6; Carrick 6.5 (Schweinsteiger 68 6.5), Schneiderlin 6; Mata 7, Rooney 6, Depay 6.5 (Young 77); Martial 7.5
Sunderland (4-2-3-1): Pantilimon 6; Jones 6, O'Shea 6, Kaboul 5.5, van Aanholt 6; Cattermole 6, M'Vila 6; Johnson 5.5 (Fletcher 45 6), Toivonen 6 (Larsson 70 6), Lens 6.5; Borini 5.5
Wayne Rooney akifurahi bao lake la kwanza la Premier League tangu mwezi April
Rooney (katikati) akikwamisha mpira wavuni
Ni bao! Wayne Rooney akiusindikiza kwa macho mpira uliotinga wavuni na kuwa bao la pili kwa United
Rooney akipongezwa na wachezaji wenzake
Comments
Post a Comment