Manchester United imeanza vibaya kampeni zake za kusaka taji la Ligi ya Mabingwa baada ya kulambwa 2-1 na PSV Eindhoven katika mchezo mkali wa kundi B.
United ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 42 kupitia kwa mchezaji wa zamani wa PSV Memphis Depay, lakini miamba hiyo ya Uingereza ikaruhusu bao la kusawazisha dakika ya 45 mfungaji akiwa ni beki Hector Moreno.
Kipindi cha pili mambo yalizidi kwenda kombo kwa United iliyokuwa ugenini baada ya kukubali bao la pili lililofungwa na Luciano Narsingh dakika ya 57.
Beki wa kushoto wa United Luke Shaw aliumia vibaya dakika ya 18 ikiaminika kuwa amevunjika mguu kufuatia rafu mbaya ya Moreno.
Shaw aliyetibiwa uwanjani kwa zaidi ya dakika tano, alitolewa nje huku akisaidiwa na mashine za kupumua.
Kwa ujumla United ilimiliki mpira kwa sehemu kubwa ya mchezo lakini ilishindwa kutengeneza nafasi za kufunga.
PSV: Zoet 6.5; Arias 5.5, Bruma 6, Moreno 5; Hendrix 6; Propper 6.5, Guardado 6 (Schaars 72, 6); Narsingh 7, De Jong 6.5, Lestienne 8 (Locadia 86).
MAN UTD: De Gea 6; Darmian 5, Smalling 7, Blind 6, Shaw 6.5 (Rojo 24, 5.5); Schweinsteiger 6.5, Herrera 6 (Fellaini 75, 6); Young 6 (Valencia 86), Mata 5, Depay 7; Martial 6.
Hii ndiyo rafu iliyommaliza Luke Shaw
Luke Shaw akipaga yowe la maumivu makali
Shaw akitibiwa uwanjani
Shaw akitolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Marcos Rojo
Comments
Post a Comment