Kocha Jose Mourinho ameagiza watu wake wa scouting kutafuta mtu ambae atam-replace Ivanovic kutokana na jinsi anavyo perform kwenye mechi za Chelsea.
Kwa muda mrefu Ivanovic alikua ni mchezaji wa kutegemewa kwenye kikosi cha Chelsea lakini sasa hivi mambo yamekua tofauti kutokana na performance yake kuwa mbovu.
Mkataba wa Ivanovic unaisha mwishoni mwa msimu huu na kuna uwezekano wa kuongezewa mkataa wa miezi 12, lakini wakati huo huo Chelsea wanaendelea kutafuta mbadala wake.
Cesar Azpilicueta alicheza kwenye left back na kuchukua nafasi ya Ivanovic wakati Chelsea ikishinda dhidi ya Maccabi.
Comments
Post a Comment