MAISHA YA VAN PERSIE NDANI YA FENERBAHCE SIO MAZURI


MAISHA YA VAN PERSIE NDANI YA FENERBAHCE SIO MAZURI

2C6ED52400000578-3243293-image-a-43_1442840231802

Licha ya kufunga goli kwenye mechi weekend hii lakini bado maisha ya mchezaji huyu sio mazuri ndani ya club hiyo.Van Persie amecheza mechi tatu bila kufunga goli ikiwemo mechi waliyofungwa magoli 3-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Mchezaji huyu mwenye miaka 32 aliweka wazi kwamba hakupenda jinsi alivyonzia benchi kwenye mechi ambayo alishinda goli la ushindi dhidi ya Bursaspor.

"Kusema ukweli sina furaha kwa sasa, sikuwa na furaha jinsi nilivyoanzia benchi wakati nilikua fit kucheza dakika zote 90. Kitu pekee ambacho nilichotakiwa kufanya kuonyesha kwamba sikupenda kilichofanyika ni kuisaidi timu yangu kushinda mechi. Ndivyo hivyo ilivyofanyika na tumeweza kupata ushindi."

Maisha ya Van Persie ndani ya club yake mpya yameanza tofauti na vile alivyotegemea lakini anaendeleak ucheza na kujitaidi kufunga magoli kama mashabiki na kocha anavyotegemea.



Comments