MAGURI: “NIKIIFUNGA SIMBA, NASHANGILIA KAMA KAWA…”


MAGURI: "NIKIIFUNGA SIMBA, NASHANGILIA KAMA KAWA…"

MaguriMchezaji Elius Maguri leo atakuwa akichea dhidi ya timu yake ya zamani wakati Stand United ambayo anaichezea kwa sasa itakapokuwa ikiikabili Simba SC kwenye uwanja wa taifa ikiwa ni mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Mguri alitemwa na 'wekundu wa Msimbazi' kwa madai kwambwa kiwango chake hakiendani na klabu hiyo ya Msimbazi na kumruhusu mchezaji huyo kujiunga na klabu nyingine ambayo anaweza kufanya kazi yake vizuri.

Tayari Maguri ameshafunga magoli matatu kwenye mechi nne za ligi kuu Tanzania bara msimu huu akiwa na timu yake mpya ya Stand United 'Chama la Wana' na amesema endapo atapata nafasi ya kufunga kwenye mchezo wa leo, atashangilia kama kawaida.

"Elius Maguri aliyekuwepo Simba na wa hivisasa ni yuleyule kwa mtu anaemfahamu Elius Maguri, hata ningekuwa Simba ningeweza kufanya vizuri kwasababu tukiangalia hata nilivyoanza msimu katika mechi za maandalizi kabla sijatoka Simba nadhani nilikuwa hivi ambavyo nafanya sasa", Maguri amesema.

"Kikubwa nafikiri ni kujituma na kusikiliza mwalimu anataka nini, watu wengi pengine labda walifikiria nitakapoondoka Simba au nitakapoenda sehemu nyingine labda ntapotea. Kisaikolojia watu wanapotoka timu kubwa wanakata tama lakini kwangu mimi naona sehemu yoyote naweza kufanya kazi kwasababu mchezaji kazi yake ni kucheza mpira kwahiyo mahali popote pale unawza kucheza na kuonesha kiwango ulichonacho".

"Mchezo wetu dhidi ya Simba utakuwa mzuri ila utakuwa na ushindani wa hali ya juu kwa maana kwamba, wachezaji wengi waliopo Stand ni wale waliokuwepo Simba".

"Sisi tuliotoka Simba tunawafahamu na wao wanatufahamu kwahiyo mchezo utakuwa ni mzuri na wenye ushindani nafikiri hicho ndio kikubwa".

 "Changamoto za mashabiki zipo hazijaanza leo wala kesho, pale utakapokuwa nao watakushangilia na unapokuwa hauponao watakuzomea ili kukutoa mchezoni lakini vitu hivyo tulishakutana navyo kwahiyo mimi nafamu ni jinsi gani ya kukabiliana navyo kwasababu sio vigeni".

"Kama ikitokea nikafanikiwa kuwafunga Simba kwenye mchezo wetu wa Jumatano (leo) nitashangilia kama nilivyofanya nilipozifunga timu nyingine".



Comments